10 Oktoba 2019 - 09:01
Rais Rouhani: Njama za Marekani za mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi ya taifa la Iran zimefeli

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njama za Marekani za mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi ya taifa la Iran zimefeli na kwamba takwimu zote na moyo na utanashati wa taifa la Iran vinaonesha kuwa, kipindi cha mashinikizo ya kiwango cha juu kimeyoyoma.

(ABNA24.com) Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njama za Marekani za mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi ya taifa la Iran zimefeli na kwamba takwimu zote na moyo na utanashati wa taifa la Iran vinaonesha kuwa, kipindi cha mashinikizo ya kiwango cha juu kimeyoyoma.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo mjini Tehran katika baraza la mawaziri na kuongeza kuwa: Wananchi wa Iran wameweza kushinda na kuzima vikwazo vya kiwango cha juu na ugaidi wa kiuchumi wa Marekani kwa kusimama midete, utanashati, kuchapakazi na kujitolea.

Amesema maadui wanakiri kuhusu uwezo, subira kubwa, kusima kidete na ustahamilivu wa taifa la Iran na kuongeza kuwa, hakuna shaka yoyote kwamba nguvu na uwezo wa Iran ya sasa ni mkubwa zaidi kuliko wakati wowote mwingine.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu pia amegusia matukio ya kikanda na kusema: Serikali ya Uturuki ina wasiwasi kuhusu mpaka wake wa kusini lakini inapaswa kuchagua njia na mbinu sahihi za kuondoa wasiwasi huo.

Rais Rouhani ameongeza kuwa, katika kikao cha vongozi wa nchi tatu za Iran, Russia na Uturuki ilitangazwa kwamba, amani katika mipaka ya kaskazini mwa Syria na kusini mwa Uturuki inaweza kudhaminiwa kwa kuwepo majeshi ya Syria na kuondoka Wamarekani katika eneo hilo.

Vilevile ameashiria shughuli ya matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein bin Ali (as) na kupongeza juhudi zinazofanywa na serikali na wananchi wa Iraq kwa ajili ya kufanikisha shughuli hiyo ya kidini. Amesema: Mkusanyiko huo mkubwa unatikisa nyoyo za Wamarekani na Wazayuni na kuwatia wahka na kiwewe.

Amesema kuwa matembezi ya Arubaini ni miongoni mwa miujiza ya historia na kuongeza kuwa: Mahudhurio ya mamilioni ya Waislamu katika mkusanyiko huo adhimu ni maonyesho makubwa ya nguvu ya kisiasa, kiutamaduni na ya kiroho.   



/129